Nafasi Mpya ya Kazi: Consular Assistant – Ubalozi wa Kenya, Dar es Salaam
Ubalozi wa Jamhuri ya Kenya nchini Tanzania unatangaza nafasi ya kazi kwa mtu mwenye sifa stahiki kujaza nafasi ya Consular Assistant katika ofisi zao zilizopo Oysterbay, Dar es Salaam. Huu ni mkataba wa mwaka mmoja (1) unaoweza kuongezwa kulingana na utendaji wa kazi.
Sifa na Vigezo vya Mwombaji
Ili uweze kufikiria kwa nafasi hii, unapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
- Elimu: Shahada ya Kwanza (Bachelor’s Degree) katika Biashara, Utawala wa Umma, Sayansi ya Jamii, au fani inayohusiana.
- Uzoefu: Angalau miaka miwili (2) ya kufanya kazi katika shirika linalotambulika (Sekta ya umma au binafsi). Uzoefu wa awali katika masuala ya Konsula (Consular role) ni sifa ya ziada.
- Lugha: Uwezo mkubwa wa kuzungumza na kuandika lugha za Kingereza na Kiswahili kwa ufasaha.
- Ujuzi wa ICT: Uwezo wa kutumia kompyuta na programu mbalimbali za ofisi.
- Nyaraka Muhimu: Lazima uwe na kibali halali cha kuishi au kufanya kazi Tanzania na Cheti cha Tabia Njema (Certificate of Good Conduct).
Majukumu ya Kazi
Msaidizi wa Masuala ya Konsula atawajibika katika maeneo yafuatayo:
- Kupokea na kuhakiki maombi yote (Pasi za kusafiria, Uraia, Vyeti vya Ndoa, Vyeti vya Kuzaliwa, n.k).
- Kutoa ushauri kwa wateja kuhusu taratibu na malipo ya huduma mbalimbali za kiserikali.
- Kuandaa nyaraka za dharura za kusafiria (Emergency Travel Documents).
- Kutunza na kusasisha daftari la Wakenya wanaoishi ughaibuni (Kenyan Diaspora).
- Kuandaa ripoti za kila siku, mwezi, na robo mwaka kuhusu mapato na huduma zilizotolewa.
- Kupokea simu na kujibu hoja za wateja kwa weledi na kidiplomasia.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Kama unakidhi vigezo vilivyotajwa, tuma maombi yako yakijumuisha Wasifu wako (CV), nakala za vyeti, namba za simu, barua pepe, na majina ya wadhamini (referees) watatu kupitia anwani ifuatayo:
Barua Pepe: consularhkchtz@gmail.com
Mwisho wa Kutuma Maombi: Tarehe 6 Februari 2026.
Kumbuka: Ubalozi wa Kenya unazingatia usawa wa kijinsia na unahimiza wenye sifa kuomba mapema. Ni waombaji watakaofuzu mchujo wa awali tu ndio watakaowasiliana nao kwa ajili ya usaili.
