Nafasi za JKT 2026: Utaratibu wa Kujiunga na Mafunzo ya Kujitolea

Nafasi za JKT 2026

Nafasi za JKT Kujitolea 2026: Maelekezo na Sifa za Kujiunga

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, amewatangazia vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani kuhusu fursa za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea kwa mwaka 2026. Mafunzo haya ni sehemu ya mkakati wa serikali kuwajengea vijana uzalendo, ukakamavu, na stadi za kazi.

Utaratibu wa Kutuma Maombi

Tofauti na taratibu nyingine, maombi ya JKT kwa mwaka 2026 yanaratibiwa moja kwa moja kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya anakotoka mwombaji. Vijana wanashauriwa kufuatilia matangazo kwenye ofisi hizo katika maeneo yao ili kuanza mchakato wa usaili.

Kipaumbele kwa Wataalamu wa ICT na Michezo

Katika awamu hii, JKT imeweka msisitizo maalum kwa vijana wenye taaluma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) pamoja na vipaji vya michezo. Makundi yanayohimizwa zaidi ni pamoja na wenye:

  • Diploma na Shahada (Bachelor) ya Computer Science.
  • Information Technology (IT) na Cyber Security.
  • Computer Engineering na Digital Forensics.
  • Vipaji vya michezo mbalimbali.

Tarehe Muhimu za Kuzingatia

Tukio Tarehe
Kuanza kwa Usaili (Mikoa Yote) 26 Januari 2026
Kuripoti Makambini (Waliochaguliwa) 27 Februari – 04 Machi 2026

Angalizo Kuhusu Ajira

"Jeshi la Kujenga Taifa halitoi ajira wala halihusiki kuwatafutia ajira vijana katika asasi za kiserikali au binafsi. Lengo kuu la mafunzo haya ni kumpatia kijana stadi za kujiari na uzalendo wa kulitumikia taifa."

Sifa na Vifaa Vinavyohitajika

Kwa maelezo zaidi kuhusu sifa za jumla (kama vile umri, elimu, na afya) pamoja na orodha ya vifaa ambavyo kijana anapaswa kuwa navyo anaporipoti kambini, tembelea tovuti rasmi ya JKT: www.jkt.mil.tz.

Post a Comment

Previous Post Next Post