Matokeo ya Al Ahly Vs Yanga Leo 23/01/2026: Vita ya Kileleni Kundi B
Leo, Januari 23, 2026, macho ya wapenzi wa soka barani Afrika yanajielekeza katika Jiji la Cairo, Misri. Miamba wa soka la Tanzania, Young Africans Sports Club (Yanga SC), wanashuka dimbani kutoatana na mabingwa wa kihistoria, Al Ahly SC, katika mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya CAF Champions League.
LIVE SCORE UPDATES
AL AHLY 2 - 0 YANGA SC
(Mchezo umemalizika)
Msimamo wa Kundi B na Umuhimu wa Mchezo
Mchezo huu ni wa dabi ya aina yake kwani timu zote mbili zinaingia uwanjani zikiwa na alama 4 kila mmoja baada ya kucheza mechi mbili. Kila timu imejikusanyia ushindi mmoja na sare moja. Mshindi wa leo atajikita kileleni mwa Kundi B na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali.
Kuhusu Wapinzani: Al Ahly na Yanga SC
- Al Ahly (Misri): Inajulikana kama "Club of the Century." Wakiwa nyumbani katika Uwanja wa Cairo International, Al Ahly wana rekodi ya kutisha kutokana na uzoefu wao mkubwa wa kutwaa mataji mengi ya Ligi ya Mabingwa.
- Yanga SC (Tanzania): Chini ya uongozi wao thabiti, 'Wananchi' wameonesha kukua kwa kiwango kikubwa katika michuano ya kimataifa. Safu yao ya ushambuliaji na nidhamu ya ulinzi itakuwa mtihani mkubwa kwa Waarabu wa Misri leo.
Muda na Mahali pa Mchezo
Mchezo utaanza rasmi saa 1:00 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT). Kwa mashabiki waliopo Cairo, mchezo unapigwa katika dimba la Cairo International Stadium lenye uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya 75,000.
Hitimisho
Je, Yanga SC wataweza kuvunja mwiko na kuondoka na alama tatu ugenini, au Al Ahly wataendeleza ubabe wao nyumbani? Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa taarifa za moja kwa moja (Live Updates) na matokeo ya mwisho punde tu mpira utakapomalizika.
