Magazeti ya Michezo Leo - Januari 21, 2026

Magazeti ya Michezo Leo - Januari 21

Tanzania Yapaa Viwango vya FIFA, Morocco Yaandika Historia

Katika viwango vipya vya soka duniani vilivyotolewa na FIFA kwa mwezi Januari 2026, timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imepanda kwa nafasi mbili na kufika nafasi ya 110 duniani. Hatua hii imetokana na kiwango bora walichokionyesha katika michuano ya AFCON 2025 nchini Morocco, ambapo walifanikiwa kutinga hatua ya 16 bora.

  • Morocco: Wamepanda hadi nafasi ya 8 duniani, ikiwa ni rekodi yao ya juu zaidi kihistoria.
  • Uganda: Wanasalia kuwa vinara wa ukanda wa Afrika Mashariki wakiwa nafasi ya 85 duniani, licha ya kushuka kwa nafasi tatu.
  • Kenya: Harambee Stars wamedorora hadi nafasi ya 113 duniani baada ya matokeo yasiyoridhisha.

Simba SC Yashusha Chuma, Clatous Chama Arejea Msimbazi

Klabu ya Simba SC imetikisa soko la usajili kwa kumtambulisha beki wa kati raia wa Ivory Coast, Ismael Olivier Toure (27) kutoka Stellenbosch FC ya Afrika Kusini. Toure anakuja kuimarisha ukuta wa Msimbazi chini ya kocha Steve Barker.

Habari kubwa zaidi ni kurejea kwa "Triple C", Clatous Chota Chama, ambaye amesajiliwa kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Singida Black Stars. Huu unakuwa ni msimu wa tatu kwa Chama kurejea Simba tangu alipojiunga nao mara ya kwanza mwaka 2018. Wakati huohuo, beki Chamou Karaboue anatajwa kuwa mbioni kuondoka klabuni hapo ili kupisha idadi ya wachezaji wa kigeni.

Yanga SC Yaichakaa Mashujaa 6-0, Yaifuata Al Ahly Kibabe

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, wameonesha umwamba kwa kuifunga Mashujaa FC mabao 6-0 katika Uwanja wa KMC Complex. Mshambuliaji mpya raia wa Angola, Laurindo Aurelio 'Depu', amefanya debut ya ndoto kwa kufunga bao na kutoa asisti katika mchezo huo.

Baada ya ushindi huo uliowapeleka kileleni mwa msimamo, msafara wa Yanga umeondoka leo alfajiri kuelekea Cairo, Misri. Wanajiandaa na pambano zito la CAF Champions League dhidi ya Al Ahly litakalopigwa Ijumaa, Januari 23, 2026.

Habari Nyingine za Kimichezo

  • Azam FC: Imelazimishwa suluhu ya 0-0 na Fountain Gate FC na kumtoa winga wake Tepsi Evance kwa mkopo wa miezi sita kwenda JKT Tanzania.
  • Novatus Dismas: Kiungo huyo wa Kitanzania ameng'ara nchini Uturuki baada ya kufunga bao muhimu na kuisaidia timu yake ya Goztepe kushinda 3-1 dhidi ya Rizespor.
  • AFCON 2027: Rais wa CAF, Patrice Motsepe, amewahakikishia Watanzania kuwa nchi za Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya, na Uganda) ziko tayari kuandaa mashindano hayo.
  • Waziri Makonda: Amekutana na Rais wa FIFA, Gianni Infantino nchini Morocco kujadili ushirikiano na uwekezaji katika miundombinu ya michezo nchini Tanzania.








Post a Comment

Previous Post Next Post