BREAKING: Seleman Mwalimu Kuondoka Simba? CR Belouizdad Yatuma Ofa Rasmi

Seleman Mwalimu Kuondoka Simba? CR Belouizdad Yatuma Ofa Rasmi

Klabu ya CR Belouizdad kutoka nchini Algeria imetuma ofa rasmi kwenda Wydad Casablanca ya Morocco kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Seleman Mwalimu.

Mwalimu, ambaye kwa sasa anaitumikia Simba SC kwa mkopo, yuko mbioni kuondoka nchini kuelekea Algeria ikiwa dili hilo litakamilika ndani ya mwezi huu wa Januari.

Mazungumzo ya Usajili Yaanza

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa mazungumzo kati ya CR Belouizdad na Wydad Casablanca yanaendelea vizuri. Ikiwa muafaka utafikiwa, Mwalimu (ambaye pia anajulikana kama Gomes) ataondoka Simba moja kwa moja ili kujiunga na miamba hiyo ya Algeria kwa mkataba wa kudumu.

Kwa Nini CR Belouizdad Imemng'ang'ania?

Kocha mkuu wa CR Belouizdad, Sead Ramovic, ndiye anayeshinikiza usajili huo. Baada ya kufanikisha saini ya Ahoua, Ramovic sasa anamtaka Seleman Mwalimu ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kuelekea mashindano ya kimataifa na ligi ya ndani.

Hatma ya Simba SC

Ikiwa dili hili litatiki, Simba SC italazimika kutafuta mbadala wa Mwalimu kabla ya dirisha la usajili la Januari kufungwa. Mashabiki wa Simba wanasubiri kwa hamu kuona kama uongozi utaruhusu mshambuliaji huyo kuondoka katikati ya msimu.


Je, unaona Simba itayumba Seleman Mwalimu akiondoka Januari hii? Tupe maoni yako hapa chini.

Post a Comment

Previous Post Next Post